BIDHAA mbalimbali zenye thamani zaidi ya Sh2 bilioni na gari
moja, zimeteketea kwa moto baada ya ghala kuu la wafanyabiashara wa Soko
la Mwanjelwa na Sido kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia jana.
Hilo ni tukio la tatu kwa soko hilo kuungua moto.
Mara ya kwanza ilikuwa Desemba 2006, baada ya soko hilo kuteketezwa na
moto na wafanyabiashara kuhamishiwa eneo la Sido ili kupisha kujengwa
upya.
Moto mwingine ulizuka tena sokoni hapo Septemba
mwaka jana na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine 20 kujeruhiwa
huku mali zenye thamani ya mamilioni ya shilingi zikiteketea.
Katika tukio la juzi, moto huo ulioanza juzi usiku saa 2:30 na kuzimwa majira ya saa kumi na moja alfajiri, unadaiwa kuwa chanzo chake ni hujuma.
Katika tukio la juzi, moto huo ulioanza juzi usiku saa 2:30 na kuzimwa majira ya saa kumi na moja alfajiri, unadaiwa kuwa chanzo chake ni hujuma.
Mkurugenzi na mmiliki wa ghala hilo, Erasto Sanga
(Usagatikwa) alisema alipata taarifa ya ghala lake kuwaka moto kutoka
kwa msamaria mwema saa tatu usiku... “Nilipofika hapa nikakuta chumba
cha kampuni ya Jambo ambao ni wapangaji wangu kinawaka moto ndipo
nikaanza kufanya mawasiliano na zimamoto.”
“Hawa wapangaji wangu hawana tabia ya kufungua
ofisi saa moja usiku, lakini jana walifika na kufungua chumba chao na
baadaye kuondoka. Walipoondoka ndipo moto ulipoanza kuwa katika chumba
chao,” alisema na kuongeza:
“Mali yangu iliyoharibika ina thamani zaidi ya
Sh600 milioni na hatua niliyochukua ni kutoa taarifa hizi polisi na
nimewaachia wafanye kazi yao,” alisema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani
alisema moto huo umeteketeza vyumba vitatu vya wafanyabiashara,
vilivyokuwa na bidhaa mbalimbali na watu wawili wanashikiliwa kwa madai
ya kuiba mali na kuzuia magari yasiingie kuokoa mali.
Kamanda Athumani alisema kulikuwa na kundi la watu
ambalo lilikuwa linawapiga mawe waokoaji na polisi.... “Nimesikitishwa
sana na kundi la watu wachache wanatumia njia ya matatizo kama haya
kujinufaisha kwa kufanya uhalifu wa kuiba mali za watu na wengine...
walidiriki hata kuwapiga mawe waokoaji na polisi na kulizuia gari la
Zimamoto lisiingie ndani kwa kuweka mawe barabarani.”
Hata hivyo, alisema wananchi na askari hao
walifanikiwa kuokoa magari yapatayo saba yaliyokuwapo nje ya ghala hilo
kwa kuyasukuma.
No comments:
Post a Comment