Thursday, November 6, 2014

KILIMO CHA UFUTA


Hivi sasa ni msimu wa kilimo Nchini Tanzania, Katika maeneo mengi sana nchini wakulima hivi sasa wanajipanga kwa kuanddaa kuanza msimu mpya wa kilimo. wengine wanalima mazao ya chakula na wengine ya biashara. kwa wale wanaolima kilimo cha ufuta kama sehemu ya zao la biashara kuna habari njema kuhusu mbegu za kilimo husika.  Siajabu kwa mkulima kuvuna magunia 15 ya ufuta yenye kilo 100 kila gunia kwa hekta. Hii inawezekana kwa kulima ufuta aina ya Lindi 02 ambayo hukomaa kati ya siku 100-110 tangu iote.Aina hii ya ufuta ina asilimia 55 ya mafuta. Hii ni habari njema kutoka kwa watafiti wa Kilimo kutoka kituo cha Utafiti Naliendele,Mtwara. 

No comments:

Post a Comment