Friday, December 21, 2012

HATIMAYE LULU MICHAEL AWA HURU.

Chama cha umoja wa waandishi wa habari kimeripoti kwamba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam asubuhi ya leo imempa dhamana msanii Elizabeth Michael baada ya kupitia vifungu kadhaa na kuona kesi yake ya kuua bila kukusudia inadhaminika.

Kwa maana hiyo, Lulu sasa
atasherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka na mwaka mpya wa 2013 akiwa na familia yake, ndugu, jamaa na marafiki.

Msanii huyo ambaye anatuhumiwa kuhusika na kifo cha msanii mwenzake, Steven Kanumba - The Great, alibadilishiwa kosa la kuua na kuwa kuua bila kukusidia, ambalo, kwa mujibu wa sheria linadhamnika na kwamba ikiwa mtuhumiwa atapatikana na hatia, adhabu ya juu kabisa ni kifungo cha maisha, miaka kadhaa au kuachiwa huru....Source Henri Kapinga Blog.

No comments:

Post a Comment