MWANAFUNZI wa darasa la sita Shule ya
Msingi Kasumulu, Kata ya Ngana, wilayani Kyela, Kaselema Mpale (14)
ameuawa kikatili kwa kuchinjwa na kitu chenye ncha kali, kisha
kunyofolewa baadhi ya viungo vyake sehemu ya mwili.
Mama mzazi wa mwanafunzi huyo, Lucia Kamnyonge
alisema tukio hilo lilitokea Februari 8, mwaka huu saa 1:30 usiku,
alipotumwa na baba yake kwenda nyumba ya jirani kuchukua mpunga ambao
ungetumika kwa chakula usiku.
Kamnyonge alisema mtoto wake hakupatikanika hadi
alipokutwa siku ya pili yake, akiwa amechinjwa na kunyofolewa baadhi ya
sehemu zake za mwili ambazo ni pua, mdomo, jicho, kuondolewa sehemu zake
za siri na kuchunwa ngozi ya kichwa karibu na utosi na mwili wake
kutundikwa juu ya mti.
Aliendelea kuwa baada ya hali hiyo taarifa
ilipelekwa ofisi ya serikali ya kijiji, uliitishwa mkutano wa wananchi
wote na walitawanyika kuanza kumtafuta mtoto huyo bila ya mafanikio.
Baadaye, baba yake alimkuta juu ya mti akiwa ametundikwa kichwa chini miguu juu na viungo vyake hivyo vikiwa vimenyofolewa.
Baadaye, baba yake alimkuta juu ya mti akiwa ametundikwa kichwa chini miguu juu na viungo vyake hivyo vikiwa vimenyofolewa.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ibungumbati
lilipotokea tukio hilo, Adam Mkese alidai tukio hilo limewashtua na
kwamba, mkutano wa kijiji ulioitishwa kwa dharura wananchi walimhusisha
baba mzazi wa mtoto huyo na mauaji hayo.
Mkese alidai watu wa kijiji hicho walimhusisha
kutokana na mazingira tata ya kifo chenyewe na maelezo ya kujichanganya
aliyoyatoa.
Ofisa mtendaji wa kijiji hicho, Naomi Charles
alidai kuna dalili za mzazi huyo kuhusishwa na mauaji hayo na kwamba,
polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi.
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Baruti Mwakasala
alidai kuwa hali katika kijiji hicho siyo nzuri na kushukuru polisi kwa
hatua za haraka walizochukua.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman
alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kukiri kumshikilia baba mzazi
wa mtoto huyo kwa uchunguzi zaidi.
No comments:
Post a Comment