HEALTH

FAHAMU MADHARA YA KUFANYA KAZI USIKU

Wanasayansi wanasema kuwa kufanya kazi katika muda usio wa kawaida kikazi au katika mazingira yaliyo ya upweke kunaweza kuzeesha ubongo na kufanya uwezo wa utendaji kuwa duni.
Utafiti huo umeeleza katika jarida la Occupational and Environmental Medicine kuwa iwapo kazi za kupokezana, mfano nyakati za usiku zitafanywa kwa takriban miaka kumi mfululizo zitazeesha ubongo kabla ya wakati wake.
Wanasayansi wanasema ahueni imeonekana kwa watu baada ya kuacha kufanya kazi hizo lakini ilichukua miaka mitano kurejea kwenye hali ya kawaida.
Utafiti huu unaelezwa kuwa muhimu, kwa kuwa waathiriwa wengi kutokana na tatizo hilo wamekuwa wakilala usingizi wa mang'amung'amu.
Athari mbaya ambazo zinaelezwa kutokana na mtindo huo wa ufanyaji kazi ni madhara ya Saratani na uzito mkubwa.Wataalam hawa wamesema kuwa miili na akili zimejengwa kwa kufanya kazi mchana na kulala nyakati za usiku.
Timu ya wanasayansi kutoka chuo cha Swansea na Toulouse wameonesha kuwa kuna madhara ya kiakili pia.

No comments:

Post a Comment