Wakati michuano ya kombe la Dunia ikiendelea nchini Brazil, timu ya taifa ya Algeria imerejea nchini humo na kupewa mapokezi makubwa kwa mashabiki wa soka nchini Algeria,

Timu hiyo ambayo ilifanikiwa kupita nakuingia katika hatua muhimu ya mashindano ya kombe la dunia katika hatua ya mtoana kabla ya kinyang'anyiro cha robo fainali za kombe la dunia iliweka historia ya taifa hilo iliyokuwa haijawahi kufikiwa na Taifa hilo.Watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Al Shabaab wameshambulia kituo cha polisi na hoteli mjini Mpeketoni, pwani ya Kenya .
Makabiliano makali yameripotiwa sehemu kubwa ya Jumapili usiku huku wakaazi wakitorokea msituni karibu na kisiwa cha Lamu. Shirika la msalaba mwekundu linasema kuwa hadi kufikia sasa watu 48 wanahofiwa kuuawa katika shambulizi hilo lililotokea usiku wa kuamkia leo. Hata hivyo vyombo vya habari vinasema idadi hiyo huenda ikawa juu zaidi. Shambulizi lilifanyika usiku wa kuamkia leo pale ambapo watu waliokuwa wamejifunika nyuso zao wakiwa wamejihami vikali walivamia vituo vya polisi , hoteli na benki. Shambulizi hilo linakuja siku kadhaa baada ya serikali ya Uingereza kufunga ofisi zake mjini Mombasa kwa hofu ya usalama. Duru za jeshi la Kenya zimearifu kuwa wapiganaji hao hawajajitambulisha ni wa kundi gani.


Kituo kimoja cha polisi kilichoshambuliwa na wapiganaji hao Baadhi ya walioshuhudia wamearifu kuwa 
wameona maiti kadhaa na majeruhi wengi japo Polisi hawajathibitisha ni watu wangapi wameuawa.Kenya 
imekumbwa na mashambulio kadhaa kutoka kwa wapiganaji wa kisomali wa Al Shabaab tangu ipeleke 
wanajeshi wake ndani ya Somalia mwaka wa 2011.Duru kutoka kisiwa cha Lamu zimearifu kuwa wapiganaji hao walifika katika malori mawili na kurusha kifaa kama bomu ndani ya kituo cha polisi kisha wakakivamia na kuiba silaha.
'Washambuliaji ni kina nani ?'
Msemaji wa Jeshi la Kenya Meja Emmanuel Chirchir ameandika katika mtandao wa Twitter kusema kuwa wapiganaji hao wameshambulia kijiji kimoja na kufyatua risasi kiholela katika kituo kikuu cha biashara.''Huenda wapiaganaji hao wakawa Al shabaab,'' ameongeza Meja Chirhir.Mmoja wa walioshuhudia amesema kuwa hoteli zilishambuliwa. "Baadhi ya hoteli zimewashwa moto hatujui watu wangapi wamejeruhiwa kufikia sasa. Tumeambiwa wameshatoroka lakini polisi wanawafuata waliko,'' alisema mtu huyo

Wakiwa katika endeo la kuingilia uwanja hapo
 
                                          baadhi wakiwa tayari wamefanikiwa kupenya ndani
Mtawa mmoja kutoka Italia ambaye alipata umaarufu katika mtandao wa kijamii ameshinda shindano la kuimba nchini humo.
Mtawa huyo, Sister Christina Scuccia alitokea kwa mara ya kwanza katika televisheni kushiriki shindano la The Voice.
Scuccia aliyeonekana amevalia mavazi yake ya utawa na msalaba shingoni, alijawa na furaha na kumshukuru Mungu kwa kumfikisha katika ushindi huo.
Mtindo wake wa wimbo wa Alicia Keys, kwa jina 'No One', https://www.youtube.com/watch?v=TpaQYSd75Ak umetizamwa zaidi ya mara milioni 50 katika mtandao wa You Tube tangu auimbe.
Mtawa huyo mwenye umri wa miaka 25 amesema kuwa aliamua kushiriki mashindano hayo kufuata ushauri wa Papa mtakatifu Francis, kuwa kanisa liwakaribie zaidi watu wa kawaida.

1. Mwili wa marehemu George Tyson utapelekwa nyumbani kwake (Mbezi Makonde jijini Dar es Salaam) kesho Jumanne Juni 3, 2014 jioni kuanzia saa kumi na mbili jioni kwa ajili ya kuaga.
 
2. Mwili utalala utalala nyumbani kwake Mbezi na kesho yake Jumatano  Juni 4, 2014 kupelekwa Viwanja vya Leaders Club kwa ajili ya kuagwa kuanzia saa nne asubuhi.
 
3. Baada ya kuagwa mwili wa marehemu utapelekwa moja kwa moja Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya kusafirishwa kwenda Nairobi  Kenya 

MWILI WA MAREHEMU GEORGE OTIENO (TYSON)UNATARAJIWA KUAGWA KESHO JUMANNE KATIKA VIWANJA VYA LEADERS NA BAADAE KUSAFIRISHWA MPAKA KISUMU NCHINI KENYA KWAAJILI YA MAZISHI YANAYOTARAJIWA KUFANYIKA HUKO TAREHE 7 JUNE AMBAPO TARATIBU ZINAENDELEA KUFANYWA NA NDUGU ZAKE PAMOJA NA MARAFIKI NYUMBANI KWAKE MAKONDE JIJINI.
 Msanii wa Hip Hop nchini, Ambwene Yessaya 'AY' (anayehesabu pesa) aliamua kujitole kununua jeneza la kusafirishia mwili w marehemu, jeneza hilo liligharimu kiasi cha shilingi laki sita ambazo AY alizitoa cash!
 wakisaidiana kubeba jeneza hilo kuelekea hospitalini baada ya kulinunua
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba (mbele), akiongozana na AY kuelekea hospitalini