Monday, November 24, 2014

Bunge kujadili Escrow kwa siku mbili

 Suala la muda mdogo wa kuwasilisha na kujadiliwa kwa ripoti hiyo bungeni umelalamikiwa na baadhi ya wabunge ambapo James Mbatia na Livingstone Lusinde walikitaka kiti cha Spika kutoa muda wa wiki nzima kujadili sakata hilo ili wamalizane nalo.
Ripoti ya sakata la ufisadi katika Akaunti ya Tegeta Escrow sasa itajadiliwa kwa siku mbili bungeni baada ya kikao cha Kamati ya Uongozi ya Bunge kukubaliana kuongeza muda tofauti na ule wa awali ambao ulikuwa ni siku moja.
Ripoti hiyo ambayo inapitiwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), awali ilitakiwa kuwasilishwa bungeni tarehe 27 wiki ijayo na kujadiliwa siku hiyo hiyo.
Baadhi ya wenyeviti wa kamati mbalimbali za Bunge ambao ni wajumbe wa Kamati ya Uongozi walisema kuwa wamejadiliana na kukubaliana kuwa muda uongezwe kwani siku moja haitoshi.
Suala la muda mdogo wa kuwasilisha na kujadiliwa kwa ripoti hiyo bungeni umelalamikiwa na baadhi ya wabunge ambapo James Mbatia na Livingstone Lusinde walikitaka kiti cha Spika kutoa muda wa wiki nzima kujadili sakata hilo ili wamalizane nalo.
Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel jana baada ya kikao cha Kamati ya Uongozi alisema ni kweli wamekubaliana mjadala huo upewe siku mbili hivyo wanaangalia jambo gani watakaloweza kulitoa kwenye ratiba ili siku hizo zipatikane.
“Wenyeviti walitoa hoja ya kutaka muda uongezwe hivyo tumekubaliana itakuwa siku mbili. Tunaangalia kitu gani kitakachotoka kwenye ratiba ili tuweze kupata hizo siku mbili,” alisema Joel na kuongeza: “Huenda ikawa kati ya Jumatano au Alhamisi wiki ijayo.”

Alisema ratiba mpya itatoka kesho (leo) kwa kuwa kuna mambo kama azimio la usalama ambayo hayawezi kuachwa kwa kuwa Tanzania imekuwa ikilaumiwa na nchi za Afrika Mashariki kuwa imechelewa kuridhia.

No comments:

Post a Comment