Thursday, April 11, 2013

PAPARA YA UMAARUFU,KUTOKUKAA CHINI YA WATU WENYE UWEZO NA MAANGAMIZI YA MAKUNDI CHANGA BINAFSI YA MZIKI WA INJILI TANZANIA

KUMEKUA NA MFUMUKO MKUBWA WA WAIMBAJI WA MZIKI WAINJILI BINAFSI WANAOIBUKA NA KUUNDA MABENDI PAMOJA NA WAO WENYEWE KUWA KAMA SEHEMU YA WASIMAMIZI WA MAKUNDI HAYO.
YAPO MAKUNDI AMBAYO YAMEFANIKIWA NA MENGINE KUVUMA KWA KIPINDI KIFUPI NA KUGAWANYIKA AMA KUPOTEA KABISA SWALI NIKUA NDANI YA HAYA MAKUNDI KUNA KITU GANI KILICHOJIFICHA?

WENGI HUSINGIZIA KUKUA KWA HUDUMA, SWALI NINALOJIULIZA NI KUWA, HIVI KWELI KUKUA KWAHUDUMA GANI HUKU AMBAKO WATU WAKITOA CD MOJA TU WANAGAWANYIKA?
KWA MTAZAMO WANGU MIMI SINA HAKIKA NA MISURI YA KISHERIA ILAYOPATIKANIKA KWA CHAMA HUSIKA KINACHOSIMAMIA WAIMBAJI HAWA KAMA KIPO NA WENYEWE PIA KAMA WANAUWEZO WA KUBEBA NA KUONGOZA HAYO MAKUNDI KUFIKIA MAFANIKIO.

WENGI NINAOWAJUA HAWAKUWEZA HATA KUJIONGOZA WENYEWE NA LEO WANASIMAMIA MAKUNDI MAKUBWA AMBAYO HAYAPO VIZURI KIMSIMAMO.

WASHIRIKI WA KUBWA WA HAYO MAKUNDI (WANACHAMA)WAMEKUA WENYE TAMAA, PUPA YA UMAARUFU USIO NA MISINGI YA MAFANIKIO, KWENYE MSTAKABARI WA MAKUNDI YAO KIASI AMBACHO UNAKUTA BAADA YA MUDA MFUPI WANAZALISHA MAKUNDI MENGINE AMBAYO UKITAZAMA KWA UKARIBU UNAONA SI SWALA LA UTUMISHI ILA NI SWALA LA UMAARUFU TU.NA KUTOKUKUBARI KUKAA CHINI YA WENGINE WENYE UWEZO WA KUWAONGOZA.


 USHAURI WANGU NI HUU. WATU KUKUBARI KUKAA CHINI YA WENGINE NA WAKATI MWINGINE KUKUBARI KUONGOZWA NA MWONGOZO AMBAO UMEWEKWA KISHERIA ILI KULIFANYA KUNDI KUWA KUNDI.WATANGAZAJI WA VITUO MBALI MBALI VYA KIINJILI KUWASAIDIA WAIMBAJI KUONA THAMANI YA KUONGOZWA NA KUSIMAMIWA NA MTU MWENYE TAALUMA YA USIMAMIZI AMA UONGOZI KWAKUANDAA PROGRAM ZINAZOHAMASISHA KUWEPO KWA USIMAMIZI BORA ILIKUFIKIA NDOTO ZAO ZA KIMAFANIKIO. MAKAMPUNI YANAYOWEZA KUDHAMINI MZIKI WA INJILI HAPA KWETU KWASASA YAPO NA MILANGO IPO WAZI KUWASAIDIA WENYE UELEKEO NA NIA YA DHATI YAKUFANYA MUZIKI WA INJILI KWA KIWANGO.

No comments:

Post a Comment