Thursday, October 18, 2012

HIVI KARIBUNI TAIFA HILI LILIADHIMISHA JUBILEE YA MIAKA HAMSINI YA UHURU LIKIWA NA SIFA NJEMA KABISA YA KUHUSIANA NA UHURU NA UMOJA ULIODUMU KWA MIAKA YOTE HIYO HAMSINI PAMOJA NA KUWAPO KWA CHANGAMOTO KADHA WA KADHA ZA UMASIKINI RUSHWA NA MAMBO MENGINI.NA WENGI TUKAAMINI KUA SASA TUNAANZA TAIFA JIPYA LENYE MALENGO MAPYA KWA KISHINDO.JAMBO LINALONISHANGAZA KUPITA KAWAIDA NI HALI YA UDINI INAYOLIVAMIA TAIFA KWAKASI YA AJABU AMBAPO MPASUKO UMEANZA KUSAMBAA KWA KASI YA AJABU KAMA UVUMI WA UPEPO.MWASWALI NAYOJIULIZA HII NDIO MIANZO MIPYA BAADA YA MIAKA HAMSINI YA UHURU WA TAIFA HILI?NA HATA LINI HAKI HUTAFUTWA KWA KUCHOMA NYUMBA ZA IBAADA NA MATISHO YA KIDINI?NAOGOPA SANA NA NAHISI KUNAKIZAZI KIPYA KISICHOJUA UTAMADUNI WETU WA TANZANIA KIMEVAMIA TAIFA LETU.SWALI WAMEFIKIAJE KIMA HIKI NA TUKASHINDWA KUWATAMBUA KAMA MAGUGU KATIKA TAIFA LETU AMBALO KIHISTORIA HALIJAWAHI KUWA NA MAMBO YA UDINI KAMA YANAVYOJITOKEZA HIVI LEO

No comments:

Post a Comment