Tuesday, March 12, 2013

UKATILI DHIDI YA WATU WAISHIO NA ULEMAVU WA NGOZI (ALBINO)


Tunaweza tukasema kwamba ukatili dhidi ya wenzetu wenye ulemavu wa ngozi(ALBINO) Tanzania umekoma?sidhani kama ni sahihi kuwaza hivyo japo yatupasa kuwaza hivyo.tatizo la kuwashambulia ndugu zetu waishio na ulemavu wangozi limekua likijitokeza mara kwa mara hapa nchini nakuweka tishio kubwa kwa familia ambazo zina watu wenye ulemavu wa ngozi nakuwafanya kuishi katika mashaka makubwa sana.hali hiyo ipo mpaka sasa Imani za kishirikina katika maeneo mbalimbali zimekua zikihusika katika ukatili huu wengi wakiamini kwamba kwakufanya Hivyo wanajiwekea mazingira ya kufanikiwa kimaisha katika maeneo yao.

zipo kampeni mbalimbali ambazo zinalenga kutokomeza Unyama huu kwa ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi ili kurudisha uaminifu katika jamii ya nchi baina ya Waishio na ulemavu wa ngozi na wale wasiokuwa na ulemavu

Na pia sote twapaswa kuwa mabalozi wa kutokomeza jambo hili ili kuwafanya ndugu zetu waishio na ulemavu wa ngozi kuishi maisha ya furaha.


No comments:

Post a Comment