Saturday, September 7, 2013

Siku moja baada ya vurugu kutokea Bungeni Kuhusu Rasimu ya Katiba..........haya ndiyo maneno ya Ezekiel Maige

Baada ya Juzi jana na leo kuendelea kwa malumbano bungeni kati ya Naibu Spika,wabunge wa CCM kwa upande mmoja na Wabunge wa upinzani kwa upande wa pili wakiongozwa na CDM,wadau mbalimbali wamekuwa wakitoa maoni yao juu ya kile kilichojiri jana wakati wa kikao cha bunge la Mchana baada ya Naibu Spika kutumia Askari wa bunge kumtoa nje kwa nguvu Mhe Sugu,hali iliyopelekea tafrani kubwa sana.

Akitoa maoni yake ktk ukurasa wa Facebook,Mh Ezekiel Maige mbunge wa Msalala alisema kuwa hakuona sababu kabisa ya kufikia hapo kwani hali hiyo ingewezwa kuepushwa.

Ingewezekana kabisa kuahirishwa kwa muswada huo na kutoa nafasi kwa kamati ya katiba na sheria kwenda Zanzibar kupata maoni ya wenzetu huko.

Najuwa kuna maelezo mazuri ya kushirikishwa kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,lakini Kikanuni baada ya muswada huo kusomwa kwa mara ya kwanza unakuwa mikononi mwa Bunge.Kamati ndio inayokusanya maoni na sio serikali.

Kwa kuwa hakuna ushahidi wa Public hearing iliyofanyika Zanzibar na kuwasikia Wazanzibari wa kawaida(nje ya serikali) basi kulikuwa na haja kabisa ya kurekebisha kasoro hiyo kwa kutoa nafasi kwa kamati kwenda Zanzibar!!

Swala la katiba ni swala kubwa hivyo ni vema zikafanyika jitihada za kutosha kuhakikisha tunakwenda pamoja(na wenzetu haswa wenye mtazamo tofauti na sisi CCM) badala ya kutumia "Wingi wetu" kwani mwisho wa safari tukienda hivi watakuwepo watakaodai kuwa katiba mpya sio yao na hivyo kuikosesha "Social legitimacy"!!

Kwa kiti (Naibu Spika) kutomsikiliza Mh Mbowe (KUB) nako kulitibua mambo bila sababu ya msingi.
Angepewa nafasi ya kusikilizwa hata kama hoja yake isingekubaliwa bado ingekuwa nafuu sana kuliko shari na aibu ya jana iliyotokea.

Tumesameheana lakini tujifunze na tujitahidi sana kwenda kwa maelewano.

Mungu ibariki Tanzania. By Ezekiel Maige mbunge wa Msalala kupitia CCM.
   

No comments:

Post a Comment