Monday, September 2, 2013

Tasnia ya Filamu Tanzania sasa imepata tamasha la kuonyesha sinema za kiswahili (Bongomovies).

MTAYARISHAJI na muongozaji Bora wa filamu Swahilihood Vincent Kigosi ‘ Ray the Greatest’ ndiyo balozi wa tamasha kubwa la filamu linalojulikana kwa jina la Dar Filamu Festival (DFF 2013) linalotarajia kufanyika tarehe 24 hadi 26 September 2013, katika viwanja vya CoICT- UDSM- Posta Kijitonyama, katika kuhamasisha wapenzi wa filamu kutazama filamu za nyumbani.

.
Vincent Kigosi
Ray akiwa katika suti kali white.
Vincent Kigosi
Ray Official Producer/ Director DFF 2013.
DFF 2013 Ray
Ray Official Producer / Director DFF 2013.
“Nimefurahia sana kuchaguliwa kuwa ni Official Producer & Director wa DFF 2013 kwani waandaaji wameona umuhimu wa kuandaa tamasha la filamu kwa filamu zinazotumia lugha ya Kiswahili kwani ndio mtaji wetu, pia ni kitu kinachotoa hamasa kwetu sisi watayarishaji kuwa na tamasha letu la filamu bara, nasupport kama mdau mkubwa,”anasema Ray. Tamasha la filamu Dar Filamu Festival 2013 litaonyesha filamu zaidi ya kumi na mbili huku kila siku filamu nne zikionyeshwa kwa kiingilio bure kabisa, DFF pia itatoa fursa kwa wadau wa filamu kupata semina za utayarishaji wa filamu kutoka kwa wataalamu wa filamu waliobobea kutoka ndani na nje, DFF 2013 imekusudia kuandika historia katika tasnia ya filamu.

No comments:

Post a Comment