Tuesday, March 4, 2014

NINI CHA KUFANYA ILI SHEREHE YAKO IWEZE KUFANA

 MARA NYINGI WATU WENGI WAMEKUWA NA MATOKEO YASIYO WAFURAHISHA MARA BAADA YA HAFLA ZAO FLANI FLANI NA HASA HARUSI NA SEND OFF, KUMEKUWA NA MWINGILIANO WA MAJUKUMU WA NAMNA YA KUPLAN SHEREHE HIZO KIASI AMBACHO WALE WALENGWA WAMEJIKUTA WAKIKUBARI MATOKEO TU NA KUACHA BORA LIENDE.
CHANGAMOTO KUBWA IMEKUWA UPANDE WA MAANDALIZI YA SHUGHULI HIZO NA MGAWANYIKO WA MAJUKUMU, KWA MFANO NANI ANAPASWA KUSIMAMIA NINI AU NANI ANAPASWA KUFANYA NINI! YEPI NI MAJUKUMU YA KAMATI NA YEPI NI MAJUKUMU YA BWANA HARUSI NA BIBI HARUSI.
SHEREHE ILI IFANE YAPASWA KUZINGATIA NAMNA YA MGAWANYIKO WA MAJUKUMU KATI YA WANAKAMATI NA WAHUSIKA WAKUU WA HAFLA HUSIKA.
KWA MFANO WAHUSIKA WAKUU YAANI BWANA HARUSI MTARAJIWA NA BIBI HARUSI WANAWEZA WAKAAMUA KUWA TUWE NA WATU 100 PENGINE KATIKA HARUSI YETU MFUMO WA KIMAJUKUMU WA WANAKAMATI UKAPINGANA NA HILO NA WAHUSIKA WAKUU HAWA WAKAJIKUTA WANAFUATA MAWAZO YA WATU WENGINE NA MWISHO WA SIKU KUKOSEKANIKA KWA USAWA NA STANDARD YA SHUGHULI KUTOFIKIA VIWANGO VYA MPANGO WALIOKUWA NAO WAHUSIKA.
HIVYO NI VYEMA KUWA NA NAFASI YA KUELEZA MAHITAJI YA WAHUSIKA KATIKA KIKAO CHA KWANZA KABISA ILI KUWA NA USAWA NA KULINDA NDOTO NA MATARAJIO YA WAHUSIKA WAKUU KATIKA HAFLA HUSIKA.
No comments:

Post a Comment