Friday, May 16, 2014

watu wanne wauawa katika mlipuko mwingine leo jijini Nairobi

 milipuko miwili imetokea karibu na Soko kubwa la nguo la Gikomba mjini Nairobi.
Soko hilo linapakana na mtaa wa Easleigh ambako wasomali wengi wanaishi na kufanya kazi.

Mlipuko wa kwanza ulitokea katika gari la abiria wakati la pili likitokea upande wa pili wa soko.
Shirika la serikali la kushughulikia majanga linasema kuwa watu 10 wamefariki na wengione zaidi ya hamsini kujeruhiwa.
Milipuko ya leo imetokea siku moja baada ya Uingereza kutoa onyo kwa raia wake wanaoishi nchini humo kurejea makwao kwa hofu ya usalama na pia baada ya tahadhari kutolewa ya kutokea kwa mashambulizi ya kigaidi nchini humo.
Gikombaa ni soko kubwa la kuuza nguo ambalo linapakana na mtaa wa Eastleigh ambako wasomali wengi wanaishi na kufanya kazi.
Kenya imekuwa ikikumba na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa wawatu wenye uhusiano na kundi la wanamgambo la kiisilamu nchini Somalia la Al Shabaab.

No comments:

Post a Comment