Wednesday, November 5, 2014

WEDDING PLANNER: WAWEZA KUWA NA WATU WA CHACHE KWA SHEREHE YAKO NA IKAWA NA UBORA ULE ULE

 Mara nyingi watu wengi wanawaza au wakati mwingine bila kutarajia wanajikuta tu kuwa na sherehe yenye watu wengi sana na wakati mwingine kunakuwa na mapungufu mengi sana kwenye sherehe husika na wengi hawajui sababu ni nini?


Kukosekanika kwa mipango sahihi ndiko kunakopelekea shughuli nyingi kukosa mwelekeo na unakuta hata mpangilio wamatukio katika picha unakuwa wa kusuasua. Mara nyingi unakuta watu wanatumia mfumo uliozoeleka sana, na kujikuta mwisho wa siku wanakua na pesa ndogo mkononi kuliko kiwango cha huduma kinachohitajika.

Unaweza kuwa na harusi nzuri au send off nzuri kwa namna unavyofikiri shughuli yako iwe, kwa mfano? uliwahi kujiuliza kwanini uhitaji watu miatatu au watu miatano wakati wachangiaji wazuri hawafiki 100? kwanini usiwe na watu mia waliojitoa vizuri na sherehe yako ukaipangilia kwa gharama nafuu na ukaondokana na stress za kudaiwa au kupungua kwa fedha ambapo kunapelekea wengi kutokuwa na furaha mara baada ya kuisha kwa sherehe?

Tafuta ndugu na jamaa wanaoweza kukuchangia kila mmoja laki moja watu 80 ambapo utakuwa mil.8 na weka akiba ya watu 20 kutoka upande wa mwanamke watakaoingia bila gharama tengeneza kadi nzuri za mwaliko za bei ndogo lkn zenye mwonekano mzuri, Tafuta ukumbi au garden ambayo inaweza kuwa ya bei ndogo, Tafuta mpambaji alie bora lkn anafanya kwa garama nafuu, kwa ujumla tafuta watoa huduma walio bora lakini wanafanya huduma zao kwa bei nafuu. Weka wasimamizi wenye uelewa na shirikisha mawazo yako kabla hawajaingia kuwajibika, Epuka kuongezea vitu ambavyo hukuviplan kabla, mfano hukuplan sherehe yako iwe na bia afu ukashawishiwa katikati ya mchakato kuweka bia lazima ikukwamishe na kuyumbisha mpangilio wako na kunabaadhi ya vitu vitapoteza ubora na kusababisha sherehe yako kutofana. Itaendelea Jumatano ijayo............................


No comments:

Post a Comment