Friday, October 12, 2012

THIS IS HOW I MET MR AND MRS TIMOTHY MUNGAI

Kwa mara ya kwanza nilikutana na Mr. Timzi(Timothy) Mungai na Miss Janet Gathoni kwa sasa ni mume na mke ilikuwa Mchana wa Tarehe 31.12.2010,tukiwa kwenye foleni ya kulipia kingilio cha kuingia kwenye msitu wa Jozani (Jozani Forest)a.k.a. Msitu wa kima wekundu..nikiwa na marafiki zangu Caleb ama Calebrity Hassan Zanga al-maarufu Zanga na Jessica au Jessie Jam.
Tukiwa tunashangaa shangaa ili tulipe vya hela nikaona Caleb anatuacha anaenda salimiana na Timzi,nikajiuliza huyu Caleb ndio kwanza hii mara yake ya kwanza kuja Zanzibar inakuwaje kufahamiana na watu tena huku mbali na nje ya wilaya ya Mjini Magharibi?..Basi ule wimbo wa Zanzibar uuh Zanzibar beautiful Island of Africaaaaa ukanijia ghafla…Then after wao kusalimiana zoezi la utambulisho likaanza Caleb akasema Huyu anaitwa Timzi na alikuwa Kiranja kwenye skuli nliyokuwa nasoma…hihihi jina Kiranja limenikumbusha mbali,halafu akaongeza kuwa hawajaonana kwa miaka mingi sana ila hatimaye wamekuja onana,We were happy then Timzi alikuwa na mdada mrembo sana pembeni yake akatutambulisha kuwa anaitwa Janeth na ni mchumba wake wamekuja Zanzibar for vacation ya Holiday Season….That was lovely for sure
 
Basi tukaanza kuchanja mbuga kuingia msituni we enjoyed being around them na wao pia waliifurahia kampani yetu..ila ubaya ama uzuri wao walikuwa wanamalizia mustakabali wa vacation yao hapo kwenye msitu kwani saa tisa kamili wanatakiwa wawe bandarini kwa ajili ya kupanda boat na kurudi Dar Es Salaam ili warudi zao Nairobi n amuda huo ilikuwa saa nane kasoro so hatukuona hiana tukapeana manamba mafacebook anwani nini wao wakaenda zao sisi tukabaki Kuexplore msitu.
 
Kilichonifanya niandike haya niyaandikayo ni furaha yangu ya kukutana na these guys na  wameweza kwa kudra za Mwenyezi Mungu kufika hapa walipo leo kwani Mwaka jana mwezi wa kumi    wali-tie their knot na kuwa Mume na Mke na sasa hivi Janet ni mama  Kijacho kwani soon ata-deliver mtoto wao wa kwanza,Ni maombi yangu kwa Mwenyezi Mungu awasaidie kina Mungai kuimaliza salama safari yao ya Ujauzito,Na pia katika maisha yao ya ndoa na familia yao wakati wanamkaribisha the new baby in their family..Viva Mungai’z Viva
 
 
 

 Janet na Timzi
 Tukiwa katika msitu wa Jozani  Kushoto ni Jessie Jam,katikati ni Janeth na kulia ni Atu
 Caleb na Timothy wakiexchange namba
 Wachumba na Classmates

 On their BIG DAY
 Hatimaye ni Mr & Mrs Mungai
 Mambo ya Pedicure na rings on their Big Day

 Waki-tie the knot katikati ya mto
Baba na Mama Kijacho

No comments:

Post a Comment