Wednesday, November 7, 2012

TIZA ZA GOSPEL RYTHM KUANZA KURUKA WIKI IJAYO:


tangu mwaka 2008 nilikua na kiu ya kufanya show ya gospel ili kuinua viwango vya wanamziki wa injiri tanzania,africa mashariki na afrika kwa ujumla.baada ya kuja na  wazo hili nilitengeneza Logo unayoiona pichani siku hiyo hiyo.na baadae 2009 nilifanya majaribia kwa kumtumia mwanadada lita chuwalo lakini haikuwa nzuri sana.baada ya hapo mwakajana nikafanikiwa kutengeneza demo ambayo iliweka tofauti na vipindi vyote vya gospel vilivyoweza kuruka katika ukanda mzima wa afrika mashariki na kukawa na changamoto ya wadhamini kutokana na kuwa wadhamini wengi walikuwa bado hawaja waza kuwekeza katika taasisi za kidini hivyo ikawa ni ngumu sana baadae nikafanya mazungumzo na uongozi wa clouds tv wakawa wamenipa fulsa ya kurusha vipindi katika tv yao na sasa naweza sema ndoto zangu zimetimia kwani tupo kwenye hatua ya mwisho ya kipindi hiki kuanza kurushwa.kawaida kipindi kabla hakijaanza kuruka hutanguliwa na kitu kinachoitwa TIZA kama sehemu ya utangulizi wa show husika kuanz au matangazo ya show yenyewe.kipindi kitakua na ambo mengi sana kwa mfano unawelewaje wanamziki wa injili tanzania na mahusiano yao kwa ijumla,vitu vingi vilivyonyuma yao mitoko yao mahusiano yao na kanisa.wanatazamajwe wanakoabudu.wanaheshimu kwao au la na mengiine mengi.baada ya siku kadhaa show itatambulishwa kwenye makanisa na vyombo vya Habari maana ni kitu tofauti kabisa kutokelezea Tanzania kaa mkao wa kula inakuja karibu nawe Gospel rythm Radha halisi ya mziki wa injiri tanzania

No comments:

Post a Comment