Tuesday, May 14, 2013

TATIZO SI UMEONA NINI AU UMEFANYA NINI? TATIZO NI NINI KINAHUBIRIWA BAADA YA HAYO YOTE KUTOKEA

KUMEKUWA NA INJILI TATA PINDI MAMBO FLANI KWENYE MAISHA YANAPOTOKEA AU KUFANYIKA,WATU WENGI SI WAHUBIRI WAZURI WA HABARI NJEMA BADALA YAKE HUWA WAHUBIRI WA HABARI MBAYA DHIDI YA YALE YALE WALIYOYAONA AU KUYASIKIA HATA KAMA HAYANA UBAYA KIIVYO.
TATIZO HILI HALIJAANZA LEO TANGU ENZI ZA MUSA KIBIBILIA WAKO WATU WALIOLETA INJILI ILIYOWASHA KWENYE MASIKIO YA WATU NA KUPELEKEA KUPOTEZA MATUMAINI KABISA, YA KUELEKEA KWENYE NCHI YA AHADI KAMA WALIVYOTARAJIA.
NIWAZI KUWA ZIPO TAARIFA AMBAZO ZIKILETWA NA MUHUBIRI HUYU ZINAWEZA LETA UCHAFUZI WA HALI YA HEWA KWA WANAOSIKIA NAKUSABABISHA PENGINE KURUDI NYUMA AU KUZIMIA MOYO KABISA.
IMEBAINIKA MARA NYINGI WATU WENGI HUDAKA KWAHARAKA SANA TAARIFA MBAYA KULIKO NJEMA,HUTAZAMA KWA HARAKA SANA TAARIFA ZA UADUI KULIKO ZA USHINDI,
KAMA SABABU ZA MAISHA  YAKO ZINATOKANA NA WAHUBIRI WALETAO HUFU JUU YAKO UWE NA UHAKI BADO MAFANIKIO UTAENDELEA KUYASIKIA TU KWA WATU WENGINE NA WEWE HUJAPATA YAFIKIA HATA SIKU MOJA.
KILA DAKIKA KUNAWEZATOKEA CHOCHOTE KIWE CHEMA AU KIBAYA MAADAMU UNAISHI KINAWEZA KUKUTOKEA.UTAJIRI AU UMASKINI UZIMA AU MAUTI,KUSHIBA AU KUKAA NJAA,AMANI AU HOFU. JIFUNZE KUTAZAMA UNAONGEA NINI BAADA YA KUTOKEA HICHO KINACHOKUSUKUMA KUHUBIRI WAKATI HUO
KAMA HUJUI KUHUSU KESHO BASI USIIDHARAU LEO.

No comments:

Post a Comment