Wednesday, October 29, 2014

Ajali Mbaya yatokea Mkoani Arusha na kusababisha vifo

Watu 9 wamefariki dunia na wawili kujeruhiwa vibaya katika ajali ya barabarani iliyotokea katika eneo la Makumira wilayani Arumeru baada ya basi dogo aina ya Hiace kugongana uso kwa uso na lori la mafuta.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Arusha Lebaratus Sabas amesema katika ajali hiyo imetokea majira ya saa Kumi jioni baada ya basi hilo dogo aina ya Nisan lenye namba za usajili T519 DBV lililokuwa likitokea jijini Arusha kwenda Usariver kuhama kwenye saiti yake na kukutana uso kwa uso na Lori hilo la mafuta lenye namba za usajili T582 ACR lilikuwa linatoka Moshi kwenda Arusha.
Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi dogo na wameziomba mamlaka zinazohusika kuongeza adhabu kwa madereva wazembe.
Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh Joshua Nassari amefika katika eneo la tukio kuungana na wananchi wengine kuokoa majeruhi na amependekeza kupanuliwa kwa barabara katika eneo hilo kama hatua ya kudhibiti ajali ambazo zimekithiri katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment