Sunday, November 2, 2014

Tabora bado si shwari kwa watu wenye albinism


Wimbi la hofu dhidi ya maisha ya watu wenye albinism limeendelea baada
Msichana Kulwa Joseph (21) mwenye Albinism mkazi wa kijiji cha usonga
 kata ya sirambo wilayani kaliua mkoani tabora, amenesurika kuuawa na 
majambazi watatu, ambapo awali walimteka Balozi wa nyumbakumi na 
kumpiga ili awapeleke kwa mlemavu huyo naye kwa kubaini nia mbaya 
akawapeleka nyumba nyingine.


akizungumza katika kituo cha kulelea yatima na wanaoishi katika mazingira 
hatarishi cha huruma kilichoko chini ya kanisa kathoriki, Binti huyo 
kulwa Joseph amesema kuwa, watu ambao hawakujulikana walivamia 
nyumbani kwa jirani na kuanza kuwapiga mjomba wake anayeishi 
nyumba ya jirani.


Mmkuu wa wilaya ya kaliua Bw Saveli Maketa ambaye alimnusuru kwa 
kumhamisha porini walipokuwa anaishi amesema kuwa hali ya maisha ya
 walemavu wa ngozi wilayani humo inaonyesha kuwa hatarishi ambapo 
amewataka wananchi kuwa na mshikamano ili kuwanusuru na hali hiyo. 


Mratibu wa chama cha wenye uremavu mkoani Tabora Bw, Focus Magwesera
 amemtaja balozi aliyejeruhiwa na majambazi hayo kwa jina la makoye meli
 ambapo katika kutaka kumnusuru mlemavu huyo, aliwapeleka majambazi hao 
kwa nyumba ya jirani, huku mwenyekiti wa walemavu wilaya ya Sirambo 
akitishiwa kuuawa.

No comments:

Post a Comment